MBARONI KWA KUNAJISI WATOTO WATOTO 3 WA SHULE MOJA

0


Mtu wenye umri wa Miaka 37 Mkazi wa Kijiji Cha Senjele Wilayani Mbozi Mkoani Songwe anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwanajisi watoto 3 katika shule ya msingi Senjele ambao Wana umri chini ya miaka 8.


Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo Alex Mkama amethibitisha kumshikilia mtuhumiwa huyo ambaye kwa nyakati tofauti ametenda kosa hilo kwa watoto hao.

Mkuu wa Shule ya Msingi Senjele Uswege Kashililika amesema tukio hilo limetokea shuleni hapo huku akikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza namna walivyobaini wanafunzi hao kufanyiwa kitendo hicho cha ukatili huku mmoja wa walio akieleza namna anavyoshirikiana na wanafunzi hao katika kuupata uhalisia ulivyokuwa na kupelekea kuwapata wanafunzi waliofanyiwa ukatili.

Kwa upande wake Mratibu wa Elimu kata ya Nanyala Ayubu Chimela amesema walifanikiwa kumfikisha kwenye vyombo vya sheria mtuhumiwa huyo huku akiahidi kuendelea kutoa ulinzi kwa watoto waliofanyiwa ukatili.

Baadhi ya wazazi wa watoto waliofanyiwa ukatili huo wametoa maoni yao kwa namna gani suala hilo limewaumiza na kuiomba serikali kuchukua hatua.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top