MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA CHAMBANI WATOA MSAADA WA CHAKULA SKULI 5 ZA JIMBO LA CHAMBANI KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE WANAOJIANDAA MITIHANI YA TAIFA 2022.

Hassan Msellem
0

Mbunge na mwakilishi wa jimbo la Chambani Kisiwani Pemba, wametoa msaada wa chakula katika skuli tano zinazopatikana katika jimbo la Chambani kwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaojiandaa na mitihani ya taifa wanaokaa kambi ili waweze kujiandaa na mitihani hiyo kwa amani.


Akikabidhi msaada huo wa chakula huko katika ukumbi wa ZSTC kwa Mtora Ukutini, Mbunge wa jimbo la Chambani Mheshimiwa Mohammed Abrahman Mwinyi, amesema viongozi wa jimbo hilo wamedhamiria kwa dhati kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa jimbo hilo kwa kutoa misaada mbali mbali ikiwemo chakula pomoka na vifaa vyakusomea.

 

“Kutolewa kwa msaada huu ni ahadi zetu ambazo tulizitoa kipindi cha kampeni kwamba endapo kama tutapata nafasi ya uongozi tutaoa msaada wa chakula kwa kila skuli ambayo ina wanafunzi wanaokaa kambi pamoja na vifaa mbali mbali kwa wanafunzi watakaofaulu ili kuongeza kiwango cha ufaulu katika jimbo letu la Chambani”

Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Chambani wakikabidhi kiroba Cha Mchele Kwa Mwalimu wa Skuli ya Sekondari Ukutini.

Nae, mwakilishi wa Jimbo hilo Mheshimiwa Bahati Khamis Kombo, amesema kutolewa kwa msaada huo ni mwendelezo wa kuisaidia sekta ya elimu katika jimbo hilo la Chambani ili kuhakikisha sekta ya elimu katika jimbo hilo inazidi kuboreka.


Mwakilishi wa Jimbo la Chambani Mheshimiwa Bahati Khamis Kombo, akizungumza na walimu, wanafunzi na kamati za Skuli wa Jimbo la Chambani katika hafla ya kukabidhi msaada huo.

Kwa upande wake, diwani wa Wadi ya Ngwachani Mohammed Said Ali, amewaomba wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo ya utolewaji wa msaada huo.


“Niwaombe sana musome kwa bidii zote ili kuhakikisha maelngo ya utolewaji wa msaada huu yanafikiwa ipaswavyo pamoja kuwatia moyo viongozi wetu ili kusudi waweze kutoa misaada kama hii kwa wanafunzi wengine” Mohammed Said Ali

Diwani wa Wadi ya Ngwachani Ndugu. Mohammed Said Ali.

Akitoa neno la Shukurani kwa viongozi hao, Mwalimu kutoka Skuli ya Msingi Mizingani Yusuf Ismail Zubeir, amesema licha misaada mbali mbali wanayoapatiwa na viongozi hao, lakini bado skuli za jimbo hilo zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kufeli kwa wanafunzi.


“Kwanza hongereni sana viongozi wetu kwa kujitoa kwenu kwa kutupatia misaada mbali mbali katika skuli zetu za jimbo la Chambani, lakini licha ya misaada hii niwaombe san sana mufanye mpango tupate walimu ukweli ni kwamba skuli za jimbo la Chambani zinakabiliwa na uhaba wa walimu hususan maandalizi na msingi hichi ni kilio kikubwa ndio maanza wanafunzi wanafeli sana” alisema

 

Mwalimu wa Skuli ya Sekondari Mizingani Yusuf Ismail Zubeir, akitoa neno la shukurani kwa viongozi wa Jimbo hilo waliotoa msaada huo.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wanafunzi wenzake, mwanafunzi kutoka skuli ya Sekondari Chambani Faki Ramadhan Faki, amesema wameshukuru sana kwa kupatia msaada huo wa chakula na kuahidi kusoma kwa bidii ili kulifikia lengo la kupatiwa msaada huo.

 

“Kwa niaba ya wanafunzi wenzangu nisema tunashukuru sana kwakupatiwa msaada huu wa chakula kwani miongoni mwa changamoto zinazotukabili kwa sisi wanafunzi tunaokaa kambi ni ukosefu wa chakula lakini kupatiwa msaada huu tuahidi kuwa tutasoma kwa bidii ili kuhakikisha lengo la kutolewa kwa msaada huu linafikiwa” Mwanafunzi

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wanafunzi wenzake mwanafunzi kutoka Skuli ya Sekondari Chambani Faki Ramadhan Faki.

Msaada huo wa vipolo vya mchele 54 na madumu 5 ya mafuta ya kupikia, umetolewa kwa Skuli tano za jimbo la Chambani ambazo ni Skuli ya Sekondari Chambani ambapo imepatiwa msaada wa vipolo 112, Skuli ya Sekondari Ukutini vipolo 37, Skulia Sekondari Mizingani vipolo 78, Skuli ya Sekondari Ngwachani 108 na Skuli ya Sekondari Wambaa vipolo 87.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top