Mchungaji wa Kanisa la Kilokole lililopo Kisesa, Nurdin Abdallah, amesomewa shtaka katika Mahakama ya Wilaya ya Magu akidaiwa Kumbaka Mtoto wake wa miaka Sita (6).
Mchungaji huyo alimchukua Mtoto kwa mama yake baada ya kutengana Julai 2022, ambapo mama wa mtoto alihamia Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, Ambapo Majirani waligundua Ukatili huo na kumpeleka Mtoto Ustawi wa Jamii.
Mtuhumiwa hakufika Mahakamani ikielezwa kuwa ni Mgonjwa hawezi kutembea.