MCHUNGAJI KANYARI ATANGAZA RASMI ANATAFUTA MKE WA KUOA

0

 Mchungaji Kanyari amefichua kuwa yeye ni mwanamume mseja anayetafuta mwanamke wa kuoa. 


Akiongea na tuko news nchini Kenya , Kanyari alisema kwamba hana haraka ya kuingia katika uhusiano lakini alikuwa na nia ya kuchumbiana na kipusa mrembo.


Kuhusiana na sura, mchungaji huyo mwenye utata alisema hana tatizo mradi apate kipusa atakayempenda na kumheshimu Miaka kadhaa baada ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Betty Bayo na mchungaji huyo mwenye utata kutengana, alisonga na maisha na kupata mwanamume mwingine ila pasta huyo hadi sasa hajatapa mchumba. 


"Mimi bado sijaoa sana. Sijapata mtu. Nitafurahi ikiwa... nitapata msichana mzuri wa kuoa,..kuna wanawake wazuri hapa nje lakini sijaamua ni yupi bado," alisema. 


Kuhusu kushirikiana katikA kuwalea wanawe na mama yao, mchungahi huyo alisema yeye hujukumikia maswala yao ya karo ya shule. "Watoto wangu wanaendelea vizuri na bado nawahudumia. Nawalipia ada ya shule. 


Kushirikiana katika malezi ya watoto hata wakati mumetengana na penzi ni sawa, kila mmoja wetu anaelewa jukumu lake katika maisha ya watoto wetu," alisema. Aliwashauri wazazi kujukumika kikamlifu kuwalea watoto wao kwa ushirikiano hata kama wametengana. "Ni vizuri kuwalea watoto uliowazaa kwani hujui kama hao utakaowapata baada ya hapo watakuwa wako au hata watakupenda au kukuchukia. 


Ukiwa na uwezo wasaidie hata wengine kadhaa." Mapema mwaka huu, Kanyari alitamba mitandaoni baada ya kumuombea aliyekuwa mwigizaji wa Tahidi High, Omosh Kizangila, ambaye alionekana kuzidiwa na Roho Mtakatifu. "Nitakuombea ili nyota yako irudi. 


Ninakupa chakula kisha kukubariki kwa KSh 7,000.” Kisura ambaye alionekana kuwa asha wa kanisani, alijitokeza na kuelekea madhabahuni akionekana kubeba mfuko uliojaa vyakula kisha kampa Omosh ambaye nusra amwage machozi.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top