MKE AKAMATWA KWA KUMJERUHI MUMEWE KWA KUSHINDWA KULIPA BILI

0

 Mwanamke mwenye umri wa miaka 23, ametiwa mbaroni baada ya kudaiwa kumshambulia na kumjeruhi mumewe mtaani Buruburu, Nairobi nchini Kenya.

Picha kutoka Maktaba


Ripoti za polisi zilibainisha kwamba Shantel Mutheu mwenye umri wa miaka 33, alimpiga Kitutu Kennedy Oshuka baada ya kutofautiana nyumbani kuhusu bili zilizokosa kulipwa.

Makabiliano yao yaliwavutia majirani waliowasikia wakipigana, na kumukoa Oshuka aliyekuwa akitiririkwa na damu.

 "Jirani aliwaambia polisi kuwa walisikia kelele kutoka kwa nyumba nambari 11 ambayo ni ya Kennedy mwenye umri wa miaka 33.

 Alikimbia hadi kwenye eneo la tukio na kukuta wawili hao wakipigana huku Oshuka akitokwa na damu," sehemu ya ripoti ya polisi kama ilivyonukuliwa na K24 Digital ilisoma.

Mwathiriwa alikimbizwa katika Hospitali ya Mama Lucy Kibaki, ambako amelazwa akiwa mahututi.

 Mshukiwa anazuiliwa na polisi huku uchunguzi kuhusiana na kisa hicho ukiendelea.

 Uchunguzi mwingine hata hivyo ulibainisha kwamba, mwanamke huyo alipandwa na mori, baada ya kugundua kwamba mpenzi wake hakuwa amelipa bili na kuanza kuvunja madirisha
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top