MOTO WA KIMAAJABU WATEKETEZA MALI ZA WANANCHI MAKETE

0

 

Wananchi wa kijiji cha Makangalawe kata ya Mang’oto  wilaya ya Makete mkoani Njombe wameeleza namna walivyoathirika na Moto uliowaka kwa zaidi ya siku tatu katika kijiji chao.

 

Wakizungumza na mtandao huu kijijini hapo wananchi hao Bw. Efeso Mgaya, Albart Mbilinyi pamoja na Patriki Malumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya maafa kijijini hapo wamesema Moto huo umeathiri Mali zao ikiwemo ekari kadhaa za Miti pamoja na eneo la malisho ya Mifugo.

 

Wamesema kuna wakati walilazimika kulala kwenye maeneo hayo yanayowaka moto ili iwarahisishie kuulima, na pia kuna wakati moto huruka umbali wa kilomita moja na kuanza kuunguza maeneo mengine lakini hadi sasa wamefanikiwa kuuzima japo kuwa hawawezi kujihakikishia kwa asilimia 100 kutokana na visiki vilivyooza ambavyo vingine vimejifukia ardhini kushika moto ambao hulipuka tena endepo kunakuwa na upepo mkali

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Makangalawe Bw Batweli Chengula amesema ni kweli wananchi wake wameathirika pakubwa na moto huo kwani mbali na kuunguliwa na miti yao pia wametumia muda mwingi kuuzima moto huo badala ya kufanya shughuli za uzalishaji mali tangu Oktoba 7 mpaka leo Oktoba 12,2022

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Makangalawe  Remijus Magere amesema Moto huo umeunguza ekari nyingi za miti ya wananchi ikiwemo waliofadhiliwa na Shirika la Pandamiti kibiashara.

 

Amesema moto huo ulisababishwa na mama mjamzito mkazi wa kijiji hicho ambaye aliwasha moto bila kibali na baada ya wananchi kufanikiwa kuuzima katika eneo mojawapo,watu wasiojulikana wakachoma moto eneo la machungio ya mifugo kati ya kijiji hicho na kijiji cha Usungilo

Chanzo;EDMO BLOG
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top