Mama wa mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho amedai kuwa aligundua tukio hilo wakati akimuogesha mtoto wake na alipomuuliza nani amefanya kitendo hicho alimtaja mtoto mwenzake kuwa anahusika
Jitihada za kumtafuta mama wa mtoto anayedaiwa kutenda kitendo hicho zimegonga mwamba baada ya kukataa kutoa ushirikiano
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Richard Thadeo Mchomvu ameitaka jamii kuishi katika mila na desturi na kuwalea watoto katika misingi ya dini ili kuepuka matukio kama hayo