Katika Kipande cha sauti alichorekodi na kukisambaza Kwenye mitandao ya kijamii, Banda anasema alimuoa mwanamke huyo miaka 13 iliyopita na kuzaa nae watoto watatu.
Aliongeza kuwa wakiwa Kwenye ndoa aliweza kujenga nyumba mbili, moja kwa ajili ya mke na nyingine kwa ajili ya mama yake kijijini kwao mwanamke.
Banda anasema mke wake alianza uhusiano na mwanaume mwingine na kuondoka nyumbani.
Alijaribu kumpigia simu lakini iliopokelewa na mwanaume jambo ambalo lilimpa hasira Banda na kupelekea uamzi wa kwenda kubomoa nyumba zote mbili ya mke na Mama mkwe kijijini.
Uamuzi huo ulikuja baada ya kugundua kuwa mwanamke amepata bwana mwingine.