Taarifa za awali zinabainisha kuwa Binti huyo alipigwa na mwanaume anaetajwa kuwa ni mume wake, Namendea Lesiria akishirikiana na rafiki yake kwa kile kilichodaiwa ni kumwaga dawa ya nyama ya mbuzi tukio ambalo limetoka Septemba 2022.
Waliofikishwa mahakamani ni mume wa binti huyo Namendea Lesiria Pamoja na rafiki yake wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Gelailumbwa Wilayani Longido Mkoani Arusha.
Kesi hiyo inasikilizwa kwa Faragha ikiwa hatua za ushahidi, na itaendelea Oktoba 20 Mwaka huu.