Waziri wa Maendelea ya Jamii jinsia wanawake na makundi maalum Dorothy Gwajima amewaangiza wakuu wa mikoa na wilaya kudhibiti mila zinazochochea ukatili wa kijinsia ikiwemo chagulaga.
Waziri Gwajima ameyasema hayowakati wa maadhimisho ya tano ya siku ya kimataifa ya wanawake wanaoishi vijijini ambayo mkoani Morogoro yamefanyika Mang'ula wilayani Kilombero.
Waziri Gwajima amezitaja baadhi ya mila hizo kuwa ni chagulaga na kutumula zinazolazimisha wanawake kuolewa bila lidhaa yao jambo linalochochea ukatili kwa wanawake.
Aidha Waziri Gwajima amesema kuwa kwanzia Januari hadi Desemba mwaka 2021 watoto 5899 walibakwa kati ya watoto 11499 waliofanyiwa vitendo vya ukatili ambapo ni sawa na wasitani wa watoto 491 walibakwa kwa kila mwezi.
Kwa upande wake Malvan Machiula Mwenyekiti wa Shujaa wa Maendeleo na ustawi wa jamii Mkoa wa Morogoro amesema wazazi wanashindwa kutoa ushirikiano mahakani pindi tunapopeleka kesi za ukatili kwa watoto mana asilia kubwa ya kesi za ukatili kwa watoto zinafanywa na watu wao wa karibu.