Wanachama cha Mapinduzi ‘CCM’ tawi la Pujini Dodo wametakiwa kujitolea katika kuunga mkono juhudi za ujenzi wa tawi hilo ili ujenzi huo uweze kukamilika kwa wakati.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwakilishi wa jimbo la Chambani Mheshimiwa Bahati Khamis
Kombo, wakati akikabidhi msaada huo wa mabati, boriti pamoja na makenchi huko
katika tawi la CCM Pujini Kichanjaani, amesema viongozi wa CCM wa jimbo hilo la
Chambani wanadhamira ya dhati ya kujenga na kuboresha matawi ya CCM, hivyo basi
amewaomba wanachama wa tawi hilo kuunga mkono juhudi za ujenzi wa tawi hilo
liweze kukamilika ujenzi wake kwa wakati.
“Sisi viongozi wenu tuna nia ya dhati katika kuhakikisha tunasaidia katika ujenzi wa matawi ya CCM katika jimbo letu la Chambani pamoja na kuyaboresha, kwahivyo niwaombe na nyinyi kuwa nia kama hiyo ili kuunga mkono juhudi hizi hususan nyinyi vijana kwasasabu nyinyi ndio nguvu kazi ya chama chetu na niwaombe muachane na propanga kuwa kujitoa katika ujenzi wa chama ni kupoteza muda” Mhe. Bahati Khamis Kombo
Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Chambani Mheshimiwa Mohammed Abrahman Mwinyi, amewasihi wanachama wa tawi la Dodo Pujini kuthamini msaada huo uliotolewa na mwakilishi ili kuwatia moyo viongozi wa jimbo hilo.
Nae, Mwenye kiti wa CCM jimbo la Chambani Ndugu Shaibu Ali Juma, amesema kutolewa kwa msaada huo ni miongoni mwa ahadi za viongozi wa jimbo hilo wakati wanaomba ridhaa ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na hatimae kutimiza ahadi hizo kwa vitendo, jambo ambalo linatia moyo na kujenga imani kwa wanachama wa jimbo hilo.
“Viongozi
wetu hawa ni viongozi wa mfano sana kwani walituahidi kutufanyia haya
wanayotufanyia leo tangu wanaomba ridhaa kwenu, na hatimae tunashuhudia leo hii
wanatekeleza kwa vitendo kwahivyo ni waombe tu ndugu wana CCM kuwaunga mkono
pamoja kuungta mkono juhudi hizi” Alisema
Othman Hassan Omar, ni Katibu wa Siasa na Uenezi Wadi ya Dodo, kwa niaba ya wanachama na Uongozi wa Tawi hilo amewashukuru viongozi wa jimbo hilo akiwemo mbunge na mwakilishi kwa kujitoa kwao katika kuwasaidia wanachama wa jimbo hilo hususan katika ujenzi wa matawi pamoja sekta ya elimu.
“Kwakweli
tunajisikia furaha kweli kweli nah ii ni faraja kwetu kwasababu ni kilikuwa ni
kilio chetu cha muda mrefu, lakini tuwashukuru viongozi wetu hawa wa jimbo letu
kwa kujitoa kwa moyo wa dhati katika ujenzi wa matawi mbali mbali pomoja na
sekta ya elimu katika jimbo hili kwakweli ni viongozi wa kuigwa” Katibu siasa
na uenezi Wadi ya Dodo
Msaada
huo umetolewa na mwakilishi wa jimbo la Chambani Mheshimiwa Bahati Khamis
Kombo, ambapo umejumuisha korija saba za boriti na makenchi, mabati pamoja na
misumari, ambapo vimegharimu shilingi milioni tano pamoja na fedha za ujenzi.