Mahakama maalumu ya makosa ya udhalilishaji Mkoa wa Kusini Pemba Chake Chake, imesema mwalimu wa skuli ya Madungu msingi Ali Makme Khatib 25, anayetuhumiwa kumbaka mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 11 anayesoma darasa la nne, anakabiliwa na kesi ya kujibu juu ya shitaka hilo.
Hakimu
wa mahakama hiyo, Muumini Ali Juma, alisema kinachoendelea juu ya mshitakiwa
huyo, ni kujitayarisha kwa ajili ya kujitetea, hasa baada ya upande wa
mashtaka, kufunga ushahidi wake.
Hakimu
Muumini, aliyasema hayo Octoba 12.2022 mwaka huu wakati mtuhumiwa huyo anayewakilishwa
na mawakili wawili dhidi ya shitaka hilo la kumbaka msichana wa miaka 11.
Hakimu
huyo, aliuuliza upande wa utetezi juu ya njia watakayotumia kufanya utetezi,
ikiwa ni ya kiapo, ambapo ukaeleza utatumia njia ya kiapo siku hiyo.
“Upande wa mashtaka tangu Octoba
11, mwaka huu ulishafunga ushahidi wake, baada ya kumsikiliza shahidi wake wa
mwisho ambaye ni askari mpelelezi, hivyo mahakama imeona mshitakiwa anayo kesi
ya kujibu” alisema hakimu Muumini
Wakili
wa mshitakiwa Suleiman Omar Suleiman, alidai kuwa wako tayari kwa ajili ya
kujitetea, juu ya tuhuma zinazowakabili mteja wao, kwa njia ya kiapo.
“Mheshimiwa
hakimu tumeshauriana sisi mahakimu na mteja wetu kuwa, siku ya utetezi
tutajitetea kwa njia ya kiapo na tunao mashahidi wetu wanne” alisema
Hivyo basi, baada ya pande zote
mbili kukubaliana, mahakama imeghairisha shauri hilo hadi Octoba 17, mwaka huu,
huku upande wa utetezi ukitakiwa kuwasilisha mashahidi wao.
Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka
Ali Amour Makame, alidai hana pingamizi yoyote na uamuzi huo wa mahakama, juu
ya kujitetea kwa mshitakiwa huyo.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo
kuwa siku ya tarehe 12.08.2022 majira ya 11:30 za jioni huko katika Skuli ya
Msingi Madungu, Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, mshitakiwa alimbaka
mwanafunzi wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 11, jambo ambalo ni kosa
kisheria kwa mujibu wa kufungu cha sheria ya adhabu nambari 6 ya mwaka 2018,
sheria ya Zanzibar.