MWAMBA AKIMBILIA KUSALI BAADA YA KUSHINDA MILLIONI 10 ZA KUBET

0

 

Kijana mmoja mpenda kandanda alifurahia mjini Lagos nchini Nigeria baada ya kushinda kitita cha shilingi Milioni 10.5 kutoka kwa Bet9ja aliyoicheza kwa shilingi 200 pekee.


Katika video hiyo iliyowafurahisha watu, wengi walikusanyika kusherehekea na kijana huyo ambaye hakuweza kuzuia hisia zake huku akibubujikwa na machozi tele.

Kwenye video hiyo iliyopakiwa kwenye mtandao wa Twitter ilimwonesha kijana huyo akisali na kushukuru mwenyezi Mungu.

Baada ya kuhakikisha ushindi wake, jamaa huyu aliyejaliwa bahati tele alikimbia kwa kasi Msikitini kwa ajili ya kutoa shukrani kwa kuneemeshwa.

Umati wa watu ulimzingira wakifurahia nao wengine wakipiga vifijo na nderemo kumshabikia mshindi huyo ambaye aliingia vitabu vya kihistoria kwa watu walioshinda pesa nyingi jimbo la kwao.

Ila cha kufurahisha ni kwamba mwanamume huyo alikuwa akijishughulisha na kurudisha shukrani kwa Mungu huku watu wakipiga kelele kwa mshangao kwa pesa alizoshinda na jinsi atakavyozitumia.

Jamaa huyu alishinda wakati ambapo Liverpool waliwashinda mahasimu wao Manchester City 1-0.

Bao la Mohamed Salah dakika ya 76 lilitosha kwa Liverpool kuibamiza Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza uliochezwa Jumapili, 16 Oktoba.

Huku Mohamed Salah aking’aa kwenye  EPL hivyo ndivyo kijana huyo aling’aa pia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top