MWANAFUNZI AJINYONGA BAADA YA MWALIMU KUMTAKA ANYOE NYWELE

Hassan Msellem
0

 

Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Langalanga, Shamamcy Wanjiru (17) amekutwa amejinyonga ndani ya nyumba yao eneo la Kaloleni Estate nchini Kenya baada ya kupewa agizo na shule kunyoa nywele zake.

Kulingana na bibi yake, Jane Wairimu, marehemu alikuwa amepewa adhabu hiyo na mwalimu wake baada ya yeye na wanafunzi wengine kukutwa wakiwa wanachana nywele zao shuleni.

Inadaiwa, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bi Rufina Nkonge alimrudisha nyumbani kwa mlezi wake kwa nia ya kujadili suala hilo baada ya kushindwa kunyoa nywele zake pamoja na barua iliyomtaka mlezi wake afike shuleni mnamo Septemba 28, 2022 ili kujadili suala la binti huyo kunyoa nywele zake.

Wanjiru alisindikizwa hadi shuleni na shangazi yake ambaye alikutana na Mwalimu mkuu na wazazi wengine ambao watoto wao walikuwa wamerudishwa nyumbani kwa sababu hiyo hiyo, kisha Mwalimu mkuu akawasisitiza watoto wao kunyoa nywele ili waruhusiwe kurudi tena shuleni.

Baada ya kurejea nyumbani anasema “nilimwacha mpwa wangu nyumbani mchana. Tulizungumza juu ya suala hilo na akakubali kunyoa. Nilimpa pesa na kumwambia afanye hivyo kwa njia ambayo angeifurahia na kukubalika na shule,”

Kwa mujibu wa shangazi, binti huyo hakuonyesha hisia zozote mbaya alipokubali kunyoa lakini baadaye walimkuta amejining’iniza na kufariki.

Ingawa familia hiyo imeweka lawama kwa uongozi wa shule, wametoa wito kwa usimamizi kuwatafuta wasichana wengine ili kuepusha vitendo kama hivyo.

“Wamenikosea. Mtoto wetu amepoteza maisha kwa sababu tu ya nywele zake alizokuwa nazo kwa miaka mitatu iliyopita. Shule inapaswa kuchukua jukumu la kutoa ushauri nasaha kwa kundi zima lililohusika,” familia imeeleza.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top