MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 12.

Hassan Msellem
0

Mahakama ya rufani Tanzania imemuhukumu kutumikia kifungo cha maisha jela mwanamke mmoja mkaazi wa Morogoro, aliyefahamika kwa jina la Shani Suleiman mwenye umri wa miaka 35, kwa kosa la kumbaka mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12.

Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo alikamatwa January 13, 2019 baada ya mama mzazi wa mtoto huyo pamoja na rafiki yake kuandaa mtego akatika nyumba ya mwanamke huyo ambapo walirekodi tukio hilo lwa kutumia simu janja.

Hii ni baada ya mtoto kumueleza mama yake kuwa mama Shani maarufu kama mama Shafii amekuwa akimuambia amuingilie mara kwa mara na wakati mwengine kinyume cha maumbile kwa kipindi cha miaka mitatu hadi kufika 2019.


Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na mtoto huyo mahakamani hapo, alidai mwanamke huyo alianza kufanya mchezo huo tangu mwaka 2016 alipokuwa darasa la tatu ambapo alimshawishi aingie chumbani kwake na siku nyengine alimpeleka katika nyumba ambayo alikuwa haijamailizika kisha kufanya kitendo hicho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top