Katika hali ya kushangaza Mwanamke mmoja anayefamika kwa jina la Grace Chacha mkazi wa mtaa wa Osunyai Jijini Arusha amelazimika kuvunja Geti na kurejesha vitu vyake ndani kwa nguvu vilivyokuwa vimetolewa nje kwenye nyumba ambayo anadaiwa aliingia kama mpangaji lakini kwa sasa akidai yeye ndiye mmiliki wa nyumba hiyo.
Alitolewa katika nyumba hiyo yenye vyumba sita vya kisasa na Neema Urio ambaye ni mke wa Ndoa wa Frank Wilbard Urio ambaye anaelezwa ndiye mmiliki wa nyumba hiyo.
Familia hiyo ya watu kumi ilitolewa katika nyumba hiyo Agosti 12, 2022 huku vitu hivyo vikikaa nje kwa muda wa zaidi ya siku kumi na wao wakilazimika kuishi kwa majirani na marafiki.
Akisimulia Tukio hilo huku akionekana mwingi wenye hasira Grace Chache anasema alihamia kwenye nyumba mwaka 2013 kwa maelekezo ya Frank Urio aliyedai alikuwa mume wake ambaye alikuwa akishirikiana naye katika biashara huku akiulamu uongozi wa serikali ya mtaa kumsusa.
Mwanaume huyo ambaye kwa sasa hajulikani alipo, Grace anasema alikuwa akimdai zaidi ya milioni 11 na ndio alipomfungulia madai mahakamani Yakiwemo ya Kindoa na kupewa haki ya kuishi kwenye nyumba hiyo bila kughasiwa huku pia akikana kujua kama alikuwa na mke mwingine.
Kwa upande wake Neema Urio anasema amefuata taratibu zote kisheria za kumtoa Grace katika nyumba hiyo ambaye yeye anamtambua kama mpangaji wake na si mkwe mwenzie.
Aidha Neema amesema alijenga nyumba hiyo Pamoja na mumuwe huku wakiwa wameiwekea malengo kupangishia watu ili kukusanya kodi za kusomeshea Watoto na jukumu la kuzikusanya alikuwa nalo mume wake.
Ndipo mwaka 2019 alipoona ada zinasuasua na kumhoji mumuwe ambaye alimpa mamlaka ya kisheria ili kuzikusanya mwenyewe.
Uongozi wa serikali ya Mtaa wa Osunyai kupitia kwa mwenyekiti wake Happy Emmanuel Kivuyo umesema Mgogoro huo ni wa Muda mrefu, ingawa zozezi la kumhamisha Grace lilifuata taratibu zote za kisheria ikiwemo ya kumpatia notisi ya kutakiwa kuhama kwa hiyari.