Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Samwel Edrew John mwenye umri wa miaka 31, mkaazi wa Welezo Unguja, ambaye ni mwenyeji wa Mkoa wa Manyara Tanzania bara, aliyekuja Zanzibar kutafuta maisha, amefariki dunia baada ya kudaiwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya nailoni.
Tukio hilo, limebainika usiku wa Octoba 19 mwaka
2022 majira ya saa 4 za usiku huko Welezo.
Mawio imezungumza na rafiki wa marehemu huyo
aliyegundua tukio hilo, amesema wakati akiwa anatoka kazini majira ya saa 4:50 za
usiku amekuta mlango umefungwa na baada ya kusukuma mlango na kufanikiwa
kuingia ndani ndipo alipokuta mwili wa marehemu ukiwa unaning’inia.
“Mimi hua nalala shamba kazini Chwaka lakini leo
nimerudi usiku wa saa 4 kama na dakika hamsini nimekuta malngo umefungwa
nikasukuma mlango ule msumari ukafunguka kuingia ndani nikamkuta mtu kanyooka
kwenye dirisha kama kajinyonga nikatoka nje nikamuamsha mpangaji mwenzangu
mmoja nikamueleza tukaenda kwa sheha na taratibu zingine zikafata” Alisema
rafiki wa Samwel
Akithibisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Elisante Makiko, amesema marehemu amekutwa
amejinyonga chumbani kwa rafiki yake anayefahamika kwa Selevesta Donald Ako.
Aidha kamanda Elisante, amesema tukio hilo la
kijana huyo kujinyonga limetokana msongo wa mawazo.
“Mtu mmoja ajuilikanae kama Samwel Endrew John
amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya nailoni chumbani kwa rafiki yake
aitwaye Selevesta Donald Ako, tukio hili la kijana kujinyonga inavyoonyesha ni
kutokana na Msongo wa mawazo, ameacha ujumbe kwamba watu wampeleke ujumbe kwa
mke wake kwamba ameamua kujinyonga lakini awatunze sana watoto Mungu akipenda
wataonana na familia mbinguni kwa Baba” Alisema Kamanda Elisante
Mwanaidi Ali Daudi, ni Mkuu wa Kitengo cha
Uhusiano hospitali ya rufaa Mnazi Mmoja, amesema mnamo majira ya saa 9 za usiku
askari wa Mwera waliufikisha mwili wa marehemu hospitalini hapo na uchunguzi
uliyofanyika haukugundua jeraha lolote katika mwili wa marehemu.
Aidha, amesema mwili wa marehemu huyo ulikuwa
unatoa harufu inayodhaniwa kuwa alitekeleza kitendo hicho cha kujinyonga siku
moja kabla na tayari mwili wake umeshachukuliwa na ndugu zake kwa ajili ya
kuanza taratibu za mazishi.
Chanzo. Kipindi
cha Mawio.