Ametoa kauli hiyo baada ya kushtushwa na taarifa aliyopewa kuhusu idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa kwa mwezi.
Akizungumza na wananchi hao wa Bukombe, Rais Samia alitoa kauli hiyo akiwata wapunguze kasi.
''Jana nimesimama Buseresere pale, nikaambiwa kituo kimoja (cha afya) kinazalisha watoto 1,000 kwa mwezi, sasa hayo madarasa baada ya miaka 3 ni mangapi?, kama ni vituo vya afya ni vingapi? tani za chakula ni ngapi,? kidogo speed (kasi) tupunguze kidogo'', alisema rais Samia.
Rais Samia aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kawaida ya kiserikali ndani ya nchi hiyo.
Katika kiwango cha sasa cha ukuaji wa idadi ya watu, idadi ya watu huongezeka mara mbili katika kipindi cha miaka 25.
Wakati ikisubiriwa taarifa rasmi ya sensa ya watu iliyofanyika mwaka huu, nchi hiyo inakadiriwa kuwa na watu zaidi ya milioni 60, kutoka kadirio la watu milioni12.5, katika miaka ya 1960.