RAIS APIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA WAGANGA WA KIENYEJI..ATAKAE KAIDI KUKIONA

0

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameamuru waganga wa kienyeji kuacha kuwatibu watu, mara moja ikiwa ni katika juhudi za kupambana na kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola.


Rais Museveni amewaamuru maafisa wa usalama kuwakamata watu watakaokaidi kuwekwa karantini wanaposhukiwa kuwa na Ebola.
 Hata hivyo hatua hiyo imechukuliwa baada ya mkutano wa mawaziri wa afya wa nchi za kikanda kujadili hali ya mlipuko wa Ebola.

Visa 54 vya maambukizi ya Ebola vimekwishathibitishwa nchini Uganda tangu kuripotiwa ugonjwa huo katika wilaya ya Mubende.

Tangu kuibuka kwa ugonjwa huo mpaka sasa watu 19 wamefariki dunia katika mlipuko mpya wa ugonjwa huo wa kwanza tangu mwaka 2019.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top