RAIS WA KENYA RUTO ATAKA KUSIWE NA MIPAKA EAST AFRIKA

0

 Rais wa Kenya William Ruto amemuomba Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akiwa kama Mzee miongoni mwa Viongozi wa Afrika Mashariki kupambana ili kuhakikisha mipaka inayotenganisha Nchi inaondolewa na kuondoa vikwazo vingine vyote ili Nchi za Jumuiya za Afrika Mashariki zisitenganishwe na mipaka na kuwe na urahisi wa muingiliano wa Watu na biashara zao.


Rais Ruto ametoa ombi hilo mbele ya Museveni leo Uganda wakati akiongea katika sherehe za kutimiza miaka 60 tangu Uganda ilipojipatia Uhuru kutoka kwa Waingereza.

“Mzee wetu Museveni una changamoto hiyo ya kutuongoza ili kuhakikisha tunaiangusha mipaka iliyoyopp na kuwe na soko huru, Wana Afrika Mashariki hatuwezi kugawana njaa au umasikini lakini tunaweza kugawana fursa na ustawi wetu, mipaka imekuwa kikwazo tuigeuze kuwa Daraja ili Watu wasafiri na bidhaa zisafirishwe kutoka Nchi moja kwenda nyingine bila masharti”

Kauli ya Ruto inakuja siku chache tangu aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Ardhini la Uganda Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye ni Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, aseme mipaka iliyopo iliwekwa na Wakoloni na hakuna haja ya kuendelea kuiacha badala yake Nchi za Afrika Mashariki zinapaswa kuifuta mipaka hiyo na kutengeneza Taifa moja.

Museveni alienda mbali zaidi na kusema ameongea na Baba yake (Rais Museveni) na kumueleza kwamba Vijana wa Afrika Mashariki wameamua Nchi za Afrika Mashariki ziungane na kuwa Taifa moja.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top