SERIKALI YAPELEKA MAJI KWA GARI KUWANUSURU WANANCHI WA VIJIJI SABA WALIOKUMBWA NA JANGA LA UKAME MONDULI

0

Serikali imeanza kupeleka Maji Kwa Magari katika Vijiji Saba Vya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha ambavyo vimekumbwa na Ukame Hali ambayo ilisababisha wakazi hao Kutumia Maji machafu yaliyotwaama kwenye mabwawa Kwa Muda mrefu huku yakihatarisha Afya zao.

PICHA KUTOKA MAKTABA ILA TAZAMA VIDEO HAPO CHINI

Mpango huo Wa dharura unagharimu kiasi Cha shilingi milioni mia Moja fedha ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania.

Wasafi Media imeshuhudia Magari makubwa yaliyobeba Maji yakitoa huduma hiyo Kwa wakazi Wa Vijiji hivyo.

Mkuu wa wilaya ya Monduli Frank Mwaisumbe akizungumza na WANANCHI ambao walifika kupokea Maji hayo amesema ni Mpango Wa Muda Mfupi wa Serikali wa kutatua Kero ya Maji Kwa Wananchi Wa Eneo Hilo.

Mhandisi Joseph Makaidi ni meneja Wa RUWASA Mkoa wa Arusha ameweka bayana kuwa SERIKALI itapeleka Maji katika Vijiji 13 vilivyokumbwa na Ukame Ndani ya Wilaya ya Monduli ikianza na Vijiji Saba.
TAZAMA VIDEO HII KUTOKA WASAF FM
Kwa Upande Wao wakazi Wa Eneo Hilo wameonyesha Furaha Yao Kwa Mpango Wa dharura Wa Serikali ila wakitaka pawepo na suluhu ya kudumu.

Wilaya ya Monduli ni miongoni mwa maeneo nchini ambayo yamekuwa shida ya Maji kutokana na kutokuwa na Vyanzo Vya chini ya Ardhi vinavyowezesha uchimbaji Wa visima Vya Maji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top