Akizungumza baada ya kikao cha uamuzi wa baraza, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Agnetha Mpangile alisema kosa hilo ni kinyume cha kanuni 42 Jedwali la 1 sehemu A(1) ya Kanuni ya Utumishi wa Umma ya Mwaka 2003, ikisomwa pamoja na kanuni D.12 na Kanuni F27(1)(a) ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma toleo la mwaka 2009.
Mpangile alisema, watumishi wengine watatu waliokuwa na masuala ya kinidhamu, baraza limeagiza wapewe adhabu ya karipio kali la maandishi.
Alisema watumishi wanapaswa kuwa na maadili ya kazi na kufuata mwongozo na nidhamu pamoja na taratibu za kiutumishi.
“Kufanya udanganyifu kwenye mambo ya fedha sio uadilifu na wala sio utumishi, hivyo ninawaasa watumishi wote, hawa ni mfano lakini kama kuna tabia ambazo zipo katikati ya watumishi wetu, basi wanatakiwa waache mara moja na kufanya kazi kwa uadilifu, vinginevyo hawa tungewachukulia hatua kubwa. Kwanza wamemdanganya mwajiri wao na halmashauri," alionya.