Shirika la Direct Aid kwa kushirikiana na taasisi ya Faraja Yetu Kisiwani Pemba, limetoa Ng’ombe wanne kwa familia mbili za wajane wenye watoto yatima ili kuwasaidia kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili.
Akikabidhi
msaada wa Ng’ombe hao, Mkurugenzi kutoka Shirika la Direct Aid Pemba Mohammed
Elsayed, amesema Shirika hilo limeamua kutoa msaada huo wa Ng’ombe kwa watu
wanaoishi katika mazingira magumu ikiwemo wajane na mayatima ili kuwapa nyenzo
zitakazowasaidia katika kukabiliana na maisha.
“Today
is a day of comfort for these families and for the leadership of Direct Aid and
Faraja Yetu institution for our families who live in difficult circumstances, we
believe that this support will be a good opportunity to develop yourself in
life inshallah” Mkurugenzi Direct Aid
Kwa
upande wake Katibu wa taasisi ya Faraja Yetu Ndugu Ali Juma Ali, amelipongeza
Shirika hilo kwa kushirikiana na taasisi ya Faraja Yetu katika kuwasaidia wananchi
wanaoishi katika mazingira magumu ikiwemo wajane, watoto yatima pamoja na watu
wenye ulemavu.
Mariam
Juma Mcha, mkaazi wa Shehia ya Chole Mwambe ni miongoni mwa wanafamilia
waliopatiwa msaada huo, amelishukuru Shirika la Direct Aid kwa kuwapatia msaada
huo wa Ng’ombe wawili na kuahidi kuwatunza ili waweze kuwa nyenzo ya maendeleo
katika maisha yake.
Nae Bi. Mayassa Mohammed Hassan, mkaazi wa Chokocho, ameliomba shirika hilo kwa kushirikiana na taasisi ya Faraja Yetu kuendelea kuwasaidia watu wanaoishi katika mazingira magumu ili nao waweze kuishi kwa furaha na amani.
“Kwakweli
tunashukuru sana sana kwa kutupatia msaada huu na tunatumai kuwa hali zetu
zitaweza kuimarika hapo baadae, ila ombi langu kwenu muendelee kuwasaidia watu
wenye hali ngumu ili nao waishi kwa furaha na amani” Alisema
Mkurugenzi wa Shirika la Direct Aid Pemba Mohammed El Sayed, akisaini mkataba wa msaada huo.
Lengo
la msaada huo ni kuwawezesha kiuchumi watu wanaoishi katika mazingira magumu
ikiwemo wajane, watoto yatima na watu wenye ulemavu Kisiwani Pemba.
Msaada
huo wa Ng’ombe wanne kwa familia mbili zenye watoto yatima, umetolewa na
Shirika la Direct Aid kutoka Nchini Kuweit kwa kushirikiana na taasisi ya
Faraja Yetu kutoka Wilaya ya Mkoani Pemba.