Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa bunge litaendelea kuiunga mkono Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa, ambayo inakuza uchumi na kuboresha utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi.
Amesema hayo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato mkoani Dodoma.
Amesisitiza kuwa Bunge litaendelea kusema 'ndio' kwenye miradi hiyo, na hivyo wananchi waelewe kuwa wanaposema 'ndio' wanasemea miradi mikubwa ya kiuchumi na kijamii.
Pia, amesema bunge litakosoa, kushawishi na kushauri Serikali pale inapobidi.
TAZAMA VIDEO HII PIA INA FURSA NZURI