TAMCODE; TUNATAKA KIFUNGO CHA MAISHA SIO KIFO

0

Shirika la Vyombo vya Habari kwa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TAMCODE) limetoa wito kwa Majaji kutoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa washtakiwa wa mauaji badala ya kifo ili kuokoa watu wasiokuwa na hatia.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMCODE, Rose Ngunangwa Mwalongo leo Oktoba 10 ikiwa ni Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani amesema TAMCODE inaungana na dunia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo ambapo kauli mbiu ya mwaka huu 2022 ni ‘Hukumu ya Kifo, Njia Iliyogubikwa na Utesaji.’

Mwalongo ameeleza kuwa kauli mbiu hii inakuja wakati ambapo dunia imeshuhudia baadhi ya shuhuda juu ya waliohukumiwa kifo kuwa walikubali makosa kutokana na kushurutishwa kwa njia za utesaji.

“Iwe ni kweli au la mchakato wa kuhojiwa unaweza kuwa na matatizo na ni vigumu sana kuthibitisha kama mtuhumiwa alitoa ushahidi kwa kushurutishwa au la. Itoshe tu kusema kuwa yapo mambo mengi ambayo yamejificha katika kila ushahidi uliotolewa”,amesema.

“TAMCODE inatambua uwepo wa Kifungu cha 197 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ambacho kinaweka bayana kuwa ‘Mtu anayepatikana na kosa la mauaji atahukumiwa kifo,’ lakini pia inatambua kwamba kumekuwepo na majaji ambao wametoa hukumu mbadala badala ya kifo, ambapo wale ambao wangehukumiwa kunyongwa, walihukumiwa kifungo cha maisha”,ameeleza.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top