UNYAMA TENA; MWANAMKE ATUPA KICHANGA CHOONI,MWENYEWE ATIWA MBARONI

0

 

Mwanamke mwenye umri wa miaka 26 amekamatwa katika eneo la Kebirigo, Kaunti ya Nyamira kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake mchanga kwenye choo cha shimo baada ya kuavya mimba.

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Nyamira Kusini, Moses Kirong alifichua kwamba mshukiwa, Maria Maroko alikamatwa na polisi siku ya Jumanne baada ya kupigiwa simu na chifu msaidizi wa Kebirigo Jackline Bware na kuarifiwa kwamba walikuwa wamemuokoa mtoto mchanga kutoka kwa choo cha shimo katika moja ya boma katika eneo la mamlaka yake.

“Nilipopigiwa simu na chifu msaidizi wa kitongoji cha Kebirigo, kikosi chetu cha maafisa kilienda katika boma hilo na kuwakuta wananchi waliomtambua mshukiwa, Maraa Maroko, ambaye alikuwa akijaribu kuavya mimba ya wiki 28 na kutupa kitoto ndani ya choo ambapo aliokolewa kutoka” alieleza Kirong.

UMETAZAMA VIDEO HII YA UKATILI WA MTENDAJI KWA WANANCHI WAKE?


Afisa huyo alisema kwamba baada ya kuhojiwa, Maria alikubali kwamba mtoto mchanga aliyeokolewa kutoka kwenye choo cha shimo ni wake. Kwa bahati mbaya, kitoto hicho kilikufa dakika chache baada ya kuokolewa.

Chifu msaidizi wa lokesheni ndogo ya Kebirigo alisema kwamba mwanamke aliyezuiliwa anatoka lokesheni ya Riakimai Bosamaro huko Nyamira na alikuwa amemtembelea dadake Ijumaa wiki jana.

"Tunashuku kuwa alitoroka kutoka kwa nyumba yake ya ndoa huko Riakimai Bosamaro ili kuja kutoa mimba kwa dada huyo," alisema msaidizi wa chifu.

Moraa atafikishwa katika mahakama za sheria za Nyamira kushtakiwa kwa jaribio la kuavya mimba; wakati huo huo, mabaki ya mtoto huyo yalipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Nyamira yakisubiri kufanyiwa uchunguzi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top