Wito huo umetolewa na mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya CCM Taifa Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, aliokuwa akizungumza katika mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa CCM Wilaya ya Domani Kichama.
Mheshimiwa Hemed, ambaye ni Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, amewahimiza wajumbe kuchagua viongozi ambao watakivusha Chama kwenye katika uchaguzi Mkuu wa Dola mwaka 2025.
Aidha amewataka wanachama kuacha majungu na fitna na makundi yasiyokuwa na tija Kwa mustakbali wa Chama sambamba na kuwataka kutoa ushirikiano Kwa viongozi wapya katika kujenga Chama imara.
Nafasi zilizogombewa katika uchaguzi huo, ni ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya, katibu wa siasa na uenezi wa Wilaya, wajumbe kumi wa halmashauri kuu ya Wilaya, wajumbe wawili wa mkutano mkuu wa Mkoa na wajumbe watatu wa mkutano mkuu Taifa.
Chanzo. ZBC RADIO