WALIMU 13 BAGAMOYO WAFUKUZWA KAZI KUTOKANA NA UZINZI, UTORO PAMOJA NA ULEVI

0

Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
WALIMU 13 wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani wamefukuzwa kazi kutokana na makosa ya utoro pamoja na wengine wanne wakijadiliwa kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kujihusisha na mapenzi na wanafunzi na ulevi uliopindukia katika kipindi cha miaka miwili kuanzia 2020 hadi sept mwaka huu.

Hatua hiyo ni fundisho kwa walimu wengine ambao wanajihusisha na tabia hizo za utoro na uzinzi.

Akizungumza katika mkutano wa chama cha walimu wilayani Bagamoyo ,Katibu wa Tume ya Utumishi TSC wilayani humo Fedinand Ndomba alisema utoro kwa baadhi ya walimu imekua ikichangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi .

Ndomba alieleza, kujihusisha mapenzi na wanafunzi sio Jambo jema kwani walimu wameaminika kulinda na kuwapa maadili mema wanafunzi hivyo walimu hao wasiwe sehemu ya kuvunja heshima Yao na miiko ya kikazi kutokana na tamaa zao.

"Walimu hususan wakiume ndio wamekuwa na tabia hii ya uzinzi na ulevi, tumepewa dhamana ya kufundisha wanafunzi tusiwe sehemu ya kukwamisha juhudi za masomo Yao" ,"alieleza Ndomba.

Ndomba alisisitiza ,hatua hiyo itasaidia kukomesha vitendo viovu vinavyofanywa na baadhi ya walimu.

Nae Mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Pwani, Douglas Mhini alieleza Chama Cha walimu hakitaweza kuwakumbatia waovu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha walimu wilaya ya Bagamoyo MKT ,Hamis Kimeze alitaja changamoto zinazowakabili walimu ikiwemo kucheleweshwa kwa fedha za uhamisho na malipo kwa wastaafu.

Katibu tawala wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni akimwakilisha mkuu wa wilaya hiyo alitumia fursa hiyo kukemea vitendo viovu vinavyofanywa na walimu na kamwe hatovifumbia macho.

"Kuna mashaka tumeyapata walimu wanapotea miezi mitatu ,mnahujumu Serikali na kuwakosesha haki wanafunzi,walimu wanaojihusisha na haya waache Mara moja,mkiona hatua kali zinachukuliwa msitafute mchawi"kwani tabia hizi ,hazipendezi,"alifafanua Kasilda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top