WALIMU WATAKIWA KUAACHANA NA MICHEZO YA KUBET

0

Walimu katika Wilaya ya Mlele Mkoani katavi wametakiwa kujiepusha na tabia ya kucheza michezo ya kubeti na kuchukua mikopo kandamizi ambayo imekuwa ikishusha heshima ya Mwalimu na utumishi wa Umma.


Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mlele ambaye pia ni katibu tawala wa Wilaya hiyo linkolin tamba wakati wa Mkutano Mkuu wa chama cha Waalimu wa Mwaka amesema

Katibu tawala ameenda mbali kwa kutoa mifano mbalimbali iyoharibu mipango ya walimu kupitia michezo ya bet ambayo ilipelekea mmoja wa mwalimu wa shule ya bweni kujikopesha fedha za wanafunzi wanazotumiwa na wazazi wao.

Tamba amesema tabia hizo zinadhalilisha taaluma ya ualimu na utumishi wa umma.

Kupitia hotuba yake aliyoisoma katibu wa chama cha Walimu wilaya ya Mlele ABDU FRANCES mbele ya mgeni rasmi wamekiri kutambua jitihada za Mhe .Samia Suluhu Hassan kuhakikisha watanzania wanakuwa na maisha mazuri ila kwa upande wa walimu mshahara ni mdogo.

Katibu tawala wa wilaya ya Mlele amekiri kupokea changamoto zao zote walizozieleza kwenye hotuba huku akisema Serikali itaendelea kuzishughulikia huku akiahidi kuhakikisha wanapatiwa eneo la ujenzi wa ofisi ya Waalimu ya Wilaya hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top