Kulingana na gazeti la Daily Monitor, mwanamke huyo kutoka nchi jirani ya Uganda mwenye umri wa miaka 59 anadaiwa kuwa mnyanyasaji sugu wa kingono.
Majirani walimkashifu mwanamke huyo kwa kuwa na tabia ya kuchumbiana na vijana. Walisema haikuwa sahihi kwake kushiriki tendo la ndoa na mvulana huyo wa miaka 19.
"Tulipoingia kwa nyumba ya mshukiwa, tuliwakuta wawili hao kitandani wakiwa uchi na wakaanza kuomba msamaha ... tuliamua kuwapeleka kwenye makao makuu ya parokia ambako tulikuta kijiji kizima kimekusanyika," Jacenta Kamashengyero, mfanyakazi wa kijamii katika eneo hilo alisema.
Gazeti la Daily Monitor liliripoti kwamba viongozi wa eneo hilo hawakutaka kumpiga mwanamke huyo lakini alichagua mwenyewe alipoombwa kuchagua kati ya kazi ya jamii na kupigwa viboko.
“Tulipowakamata wawili hao, tuliangalia adhabu zote; kazi ya jamii na kupiga viboko. Katsigaire alichagua kupigwa viboko na tukaamua kumpa viboko 10 kama onyo kwa wanawake wengine [wenye umri mkubwa],” Bigirwa alisema.
Mwenyekiti wa Kaunti Ndogo ya Kyeizoba, nchini Kenya Victor Taremwa pia alitetea adhabu iliyotolewa kwa mwanamke huyo akisema ilikusudiwa kumpa adabu.
Inaripotiwa kwamba mwanamke huyo alitoweka kutoka kijijini hicho baada ya tukio hilo la kutia aibu.