PICHA YA DC KISSA KASONGWA NJOMBE |
Wananchi wa kijiji cha Igombola kata ya Lupembe wilayani Njombe wameomba serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kuondoka na mganga wa zahanati ya kijiji hicho wakimtuhumu kukosa nidhamu, ulevi pamoja na kushindwa kutibu wagonjwa mpaka watoe fedha za matibabu wakiwemo wazee.
Katika mkutano wa hadhara wa Mkuu wa wilaya hiyo wakati akisikiliza kero pamoja na kukagua miradi ya maendeleo ,wananchi wamedai kuwa daktari Samweli Tupa amekuwa na changamoto zinazopelekea vifo kwa wagonjwa hali inayowafanya kuwa na wasiwasi mkubwa wa maisha yao ndio maana wamefikia hatua ya kuomba aondolewe.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa akamtaka mganga mkuu wa wilaya kutoa majibu ya swala hilo ambapo amesema tayari daktari huyo ameshapewa barua ya kumzuia kutibu watu, lakini mkuu wa wilaya akamtaka mganga mkuu aondoke naye kwa kuwa analeta kero kwa wananchi.