WANANCHI WASUSIA MSIBA WA MTENDAJI WAO
14 October
0
Wananchi wa mtaa wa Kabuyobo uliopo kata ya Kasamwa mjini Geita wamesusia kushiriki msiba wa Afisa mtendaji wa kata ya Kasamwa aliyekuwa akitambulika kwa jina la Japhet Maganga kwa madai kwamba enzi za uhai wake alikuwa hashiriki misiba.
Daudi Makungu ni Mwenyekiti wa maafa katika eneo hilo amekiri kuwazuia wananchi kutoshiriki shughuli za msiba huo kutokana na marehemu kutoshirikiana na Wananchi kwenye misiba kwa kipindi cha miaka mitatu.
Tags
Share to other apps