WANAUME WAWILI WAUAWA WAKIMGOMBANIA KHADIJA
01 October
0
Watu wawili waliotambulika kwa majina ya Ibrahimu Shaban (21) na Musa Bakari (28) wamefariki dunia wilayani Masasi mkoani Mtwara, baada ya kupigana kwa kutumia magogo wakati wakigombea mpenzi wao aitwaye Khadija Msamati.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi ACP Nicodemus Katembo amesema tukio hilo limetokea Septemba 29, 2022 majira ya saa sita usiku katika kijiji cha Mkangaula kata ya Namalenga wilayani Masasi.
ACP Katembo amesema tukio hilo limesababishwa na wivu wa mapenzi na baada ya kufanyika kwa uchunguzi wamebaini marehemu hao walikuwa kwenye ugomvi wa kugombea mpezi wao ambaye baada ya tukio hilo alitoweka na kwenda pasipojulikana.
Tags
Share to other apps