Serikali imesema itaendelea kuwekeza kwenye mifumo ya TEHAMA ili wananchi wote waweze kunufaika na fursa zilizopo kwenye uchumi wa kidigitali.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Mwanamke na Vikoba 2022 katika Ulimwengu wa Kidigitali.
Waziri Nape amebainisha kuwa pamoja nia njema ya serikali kuwekeza kwenye TEHAMA ili kurahisisha huduma kwa wote ni vyema wananchi watumie mitandao hiyo vizuri kwa ustawi wa maendeleo yao na Taifa Kwa ujumla.
Pamoja na mambo mengine ameagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kukutana na makampuni ya simu nchini ili kuona namna bora ya kuwawezesha wajasiriamali wanawake kwa vifurushi gharama katika kutangaza bidhaa zao ulimwenguni.
Kwa upande wake mwanyekiti wa wajasirimali hao Janeth Mahawanga ameishukuru serikali kwa kuja na mpango huo na kwamba utakuwa wa manuafaa makubwa katika kuwainua wanawake na kukuza bishara zao.
Zaidi ya wajasiriamali wanawake 100 kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam wamehudhuria kungamano hilo lililoambatana na utoaji wa elimu.