Watu hao wameuawa katika Kijiji cha Wasa Wilaya ya Iringa na katika tukio hilo, wanafamilia sita wamejeruhiwa na Watuhumiwa hao wa ujambazi. Mmoja wa aliyeuawa ni mtoto wa marehemu Mavika.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi (ACP) Allan Bukumbi, akizungumza na waandishi wa habari jana alisema tukio hilo lilitokea usiku baada ya vijana Matatizo Mavika na Christian Mavika kudaiwa kukodi majambazi kutoka Mafinga wilayani Mufindi ili kutekeleza uvamizi huo.
Bukumbi alisema vijana hao walifanya uvamizi huo baada ya kupokea taarifa zisizo sahihi kuwa Mzee Mavika ametumiwa kiasi kikubwa cha fedha na mtoto wake, Tedy Mavika, anayeishi Dar es Salaam.