WATUHUMIWA WAWILI WA UPORAJI DAR ES SALAAM WAUAWA

0

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na Wananchi wa maeneo ya Gongo la Mboto wamewadhibiti Majambazi wawili waliokuwa na silaha ya moto baada ya kufanya tukio la uhalifu wa kupora fedha Tsh.Milioni 1.5 maeneo ya Chanika.


Hata hivyo, Majambazi hao akiwemo mmoja aliyefahamika kwa jina la Kulwa walifariki dunia wakati wanapelekwa Hospitali kupatiwa matibabu kutokana na kipigo walichokipata kutoka kwa Wananchi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea October 26, 2022 saa 5:30 asubuhi ambapo Wahalifu hao walipora fedha hizo kutoka katika Kikundi cha Wakina Mama Chanika waliopewa fedha hizo kutoka Taasisi ya ASA.

"Ilipofika saa 5:30 asubuhi wakawa wamekusanya zile fedha zikawa zimefika Milioni Moja na Laki tano wakati wamekaa wakisubiri Mtu azichukue zile pesa wakatokea Majambazi wawili wakiwa kwenye pikipiki namba MC714CLL wakatishia kwa silaha wakapora zile pesa wakaondoka”

Mmoja wa wanakikundi akapiga kelele za mwizi, kipo Kikundi cha Bodaboda cha Ulinzi Shirikishi wakaanza kuwakimbiza mpaka hapa Gongolamboto yule mmoja wa Wahalifu alijaribu kupiga risasi ila akashindwa, yupo Dereva mmoja akawablock wakaanguka na mmoja akadhibitiwa na mwingine akakimbia na silaha akadhibitiwa na walishambuliwa sana wakati wa ukamatwaji”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top