Waziri Mkuu alisema mrithi wake atachaguliwa katika shindano la uongozi la chama cha Tory, litakalokamilika wiki ijayo.
Wabunge wa Tory walimsihi Bi Truss aondoke baada ya serikali yake kukumbwa na misukosuko ya kisiasa, kufuatia kupuuzwa kwa sera zake nyingi za kiuchumi.
Katika hotuba nje ya Mtaa wa Downing, Bi Truss alisema Chama cha Conservative kilimchagua kwa jukumu la kupunguza ushuru na kukuza ukuaji wa uchumi.
Lakini kutokana na hali hiyo, Bi Truss alisema: "Ninatambua kwamba siwezi kutekeleza mamlaka ambayo nilichaguliwa na Chama cha Conservative."
Bi Truss alisema atasalia kwenye wadhifa huo hadi mrithi atakapochukua rasmi wadhifa wa kiongozi wa chama na atateuliwa kuwa waziri mkuu na Mfalme Charles III.
Jeremy Hunt - ambaye aliteuliwa kuwa kansela wiki jana - amesema hatasimama katika kinyang'anyiro cha uongozi kuwa waziri mkuu ajaye.
Bi Truss - ambaye aliingia madarakani siku 44 zilizopita - atakuwa Waziri Mkuu aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi katika historia ya Uingereza
Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer aliitisha uchaguzi mkuu mara moja kufuatia hotuba ya Bi Truss ya kujiuzulu.
Katika hotuba yake, Bi Truss alisema aliingia "ofisini wakati wa machafuko makubwa ya kiuchumi na kimataifa", huku vita vikiendelea nchini Ukraine na gharama za maisha zikiongezeka.
Lakini kujiuzulu kwake kunakuja baada ya waziri mkuu, katibu wa zamani wa mambo ya ndani Suella Braverman, kujiuzulu na wabunge wa Tory kuasi katika kura ya bunge iliyokumbwa na machafuko