Serikali Wilayani Momba Mkoani Songwe imesema katika Mji wa Tunduma kumekuwa na msongamano mkubwa na Malori ambayo yamepaki barabarani na kushindwa kuvuka kuelekea kusini mwa Afrika kupitia Mpaka wa Tunduma ni kutokana na upande wa Nchi jirani Zambia kutumia mda mrefu mpakani hapo hadi kuruhusu gari kuendelea na Safari hali inayopelekea kuendelea kuwepo na msongamano wa magari barabarani.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Fackii Lulandala kufuatia uwepo wa malori zaidi ya 200 kukwama kuvuka na kusababisha uwepo wa msongamano katika Mji wa Tunduma.
Awali madereva wa malori walisema kufuatia msongamano huo umewapelekea kukaa muda mrefu kwenye foleni bila kufanikiwa kuvuka na kuiomba serikali kuingilia Kati sakata hilo kwani imekuwa ni kero kwao na kwa watumiaji wengine wa Barabara.
CC Wasafifm