Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman, leo Oktoba 04, 2022 amejumuika na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Siasa, dini na wadau kutoka ndani na nje ya Tanzania, wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kushiriki katika Ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Demokrasia Kujadili Masuala Mahsusi Ya Zanzibar Yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa.
Mkutano huo Umefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar, mbapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Oktoba 04, 2022.