Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Njombe Kassim Ephrem amesema mtuhumiwa alikamatwa November 9 mwaka huu mara baada ya kupata taarifa kwa raia mwema na kuandaa mtego uliosaidia kumkamata mtuhumiwa.
“Tumemfungulia kesi afisa kilimo wa kata kwa kudai rushwa kwa mwananchi asajiliwe kwenye kitabu ili aweze kupata namba akachukue mbolea ya ruzuku halafu yeye ni afisa kilimo wa kata hata ukimuangalia mkulima unaona dah”amesema Kassim Ephrem.
Ametoa wito kwa kuacha vitendo hivyo kwa kuwa serikali ina nia njema ya kuwasaidia wananchi hivyo hawataweza kusita kumchukulia sheria mtumishi yeyote anayekwenda kinyume na sheria.
USIACHE KLUTAZAMA VIDEO HII