AJALI NYINGINE YAUA SITA KITETO

0

 Watu sita wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea eneo linaloitwa pori namba moja Wilayani Kiteto Mkoani Manyara ikihusisha gari la Wagonjwa (Ambulance) kugongana uso kwa uso na Prado.

PICHA KUTOKA MAKTABA


Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema majeruhi watano wamepelekwa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi huku majeruhi wawili wakibaki katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

"Gari moja la kituo cha afya Sunya lilikuwa linatokea Kibaya kupeleka Mgonjwa na baada ya kumshusha Mgonjwa likawa linarejea kwenye kituo chake Sunya lakini bahati mbaya limegonga uso kwa uso na gari aina ya Prado ambayo ilikuwa inatokea upande wa Kilindi inakuja upande wa Kibaya"

DC Batenga amesema wote waliofariki katika ajali hiyo walikuwa kwenye gari la Wagonjwa (Ambulance).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top