Mwanamitindo na mfanyabiashara Kimberly Flores, amefunguka na kudai kwamba ana mazoea ya kunusa chupi za mumewe mwimbaji Edwin Luna, kubaini iwapo ana uhusiano nje ya ndoa.
Mwanamitindo
huyo wa Guatemala, alidai aliamua kuchukua hatua hiyo, katika juhudi za
kuhakikisha mumewe anasalia mwaminifu kwake.
Kimberley alidao
kwamba kunusa chupi za mumewe kutampa ushahidi iwapo ana mpango wa kando.
Na sio hayo tu,
Kimberley alisema kwamba yeye hupitia ukurasa rasmi wa Instagram unaomilikiwa
na mumewe, ili kupitia jumbe kuona iwapo kuna mwanamke anayeweza kutishia ndoa
yao.
Pia, yeye
huangalia iwapo ametumia pesa zake kwa wanawake wengine.
“Mimi huangalia
iwapo ametumia credit card kuwanunulia watu wengine vitu, niangalie pia
amempigia simu nani usiku wa manane, na hata kunusa chupi zake na kufuatilia mitandao yake ya kijamii kama
vile Instagram,” Kimberley alisema.
Mwanamitindo huyo alisema kwamba kufikia sasa,
mumewe ni mwaminifu.
Kauli hiyo ilizua hisia mseto huku wengine wakiona tabia yake Kimberley ya kunusa chupi, kuwa ni upuzi wa kutaka kumthibiti mumewe.