ALIYEKUWA KOCHA WA SIMBA SC AFIKISHWA MAHAKAMANI

0

 

Aliyekuwa kocha wa makipa wa Klabu ya Simba Muharami Sultan (40) na wenzake 6 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za usafirishaji wa madawa ya kulevya.


Mashitaka hayo yamesomwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Grace  Mwanga mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Merry Mrio na Wakili wa utetezi Daudi Mzeri.

Wengine ni pamoja na Mmiliki wa Kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zuberi seif, Said Matwiko mkazi Magole, Maulid Mzungu maarufu mbonde (54) mkazi wa kisemvule na John John maarufu Chipanda (40) ambaye jukumu lake kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka Cambiasso Sport Academy na Sara Joseph.

Mwanga ameieleza mahakama kuwa watuhumiwa wanakabiliwa na mashitaka mawili ya usafilishaji wa madawa ya kulevya

Katika hati ya mashitaka imeeleza kuwa mnamo tarehe 27,2022  Ilala Dar es Salaam walikutwa wakisafirisha madawa ya kulevya aina heroin yenye uzito wa kiliglamu 27.1.

Pia shitaka la pili wanatuhumiwa kulitenda mnamo tarehe 4,11 2022 ndani ya Wilaya ya  Mkuranga Pwani walikutwa wakisafirisha madawa aina heroin yenye uzito wa kiliglamu 7.79.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo Hakimu Mrio amewaeleza watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwani Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikilizwa kesi hiyo.

Wakili Mwanga ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado unaemdelea.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Desemba 5,2022 kwa ajili ya kutajwa na watuhumiwa wamerudishwa rumande.

TAFADHALI KAMA HUJATAZAMA VIDEO HII BOFYA SASA KUTAZAMA.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top