ALIYEOKOTA HUNDI YA KAMPUNI YA MIL 484 ALIPWA PIPI KAMA SHUKRANI

0

 Mwanamume Mjerumani mwenye jicho pevu aliyeokota hundi yenye thamani ya shilingi milioni 484 ya kampuni ya peremende, ametunukiwa pipi zenye gharama ya KSh 859. 

Anouar G mwenye umri wa miaka 38, kutoka Frankfurt aliokota hundi ya kampuni ya Haribo kwenye kituo cha gari la moshi alipokuwa akielekea kumtembelea mamake.

Wakati Anour G, alipowasiliana na kampuni hiyo kuhusu kupatika kwa hundi hiyo yenye thamani kubwa, alisikitika kwa kuzawadiwa peremende. 


Aliwaambia wanahabari kwamba: 'There was such a large sum on it that I couldn't even pronounce it.' Mail Online iliripoti kwamba hundi hiyo ilikabidhiwa na na duka kuu la Rewe kwa kampuni hiyo ya peremende ila ikapotea kwenye kituo cha treni. 


Kwa mujibu wa vyombo vya habari, wakati Anouar alipowasiliana na Haribo, mmoja wakili wake alimhimiza aiharibu hundi hiyo, na kumtumia ushahidi. Jamaa huyo alifanya alichoagizwa na siku chache baadaye, alipokea boksi kutoka Haribo iliyokuwa na pakiti 6 za premende.


Inadaiwa Anouar hakupendezwa na zawadi hiyo, kwa kuwa aliamini aliokoa kampuni hiyo kutopoteza mamilioni ya pesa. Alisema: 'I thought that was a bit cheap.'

Chanzo: TUKO.co.ke

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top