AMUUA MWENZAKE KISHA KUGEUZA KITOWEO

0

 LAZARO ADAMSON (40) mkazi wa Kaloleni wilayani Songwe, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Songwe kwa kumuua Berta Shugha (69), na kisha kuukata kata mwili wake vipande vipande na kuuchoma na kuanza kuula kama mishikaki.


Mkuu wa Wilaya hiyo Simon Simalenga amesema mtuhumiwa alidai kwamba alimuua mwanamke huyo kwa kumpiga panga kisogoni na katikati ya kichwa na kwamba alipopoteza maisha ndipo akaanza kumkata kata.

“Alisema baada ya kumuua alimkata nyayo za miguu yote, akatoa utumbo na kuukamulia kwenye beseni na yeye anadai kuwa alianza kula kwa vile alikuwa na hamu ya nyama,” amesema DC Simalenga.

Awali baadhi ya viungo vya marehemu havikujulikana vilipo na baadaye vilipatikana “Baadhi ya viungo ambavyo vilikuwa havionekani kama vile mapaja, hatimaye Askari wetu wa Jeshi la Polisi wamevipata vikiwa vimefichwa katika shimo la choo ambacho kilikuwa hakitumiki, viungo hivyo vimepatikana vikiwa vimechomwa na katika hali ya kushangaza mtuhumiwa alianza kula nyama hiyo mbele ya Askari,” ameongeza Simalenga.

NA EDMO TV.

TAZAMA VIDEO HII KABLA YA KUFANYA BIASHARA MTANDAONI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top