Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia Zawadi Msagaja mkazi wa Kijiji cha Mahaha wilayani Magu aliyemzika mtoto wake akiwa hai kwa kile kinachoelezwa kuwa aliamriwa na shemeji yake ambae ni mganga wa kienyeji amtoe kafara mtoto huyo mwenye umri wa miezi miwili ili apate utajiri.
Katika tukio lingine lililotokea tarehe 18 mwezi huu usiku katika Kijiji cha Bujingwa wilayani Kwimba mwanamke mmoja aitwaye Kahabi Kazimili aliuawa kwa kuchomwa na kisu eneo la kidevu na mumewe aitwaye Nyanda Thomas na badae mwanaume huyo kukimbia
"Msako mkali ulifanyika ndipo tarehe 21 mtuhumiwa alikamtwa akiwa mafichoni mkoani Kagera na kwamba upelelezi utakapokamilika atafikishwa mahakamani"
Tukio lingine la tatu kamanda Mutafungwa amesema katika kisiwa cha Nyamango, Kijiji cha Soswa wilayani Sengerema Shabani Ally mvuvi aliuawa baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali na rafiki yake aitwaye Mnanka Paul
"Baada ya kufanya uhalifu huo mtuhumiwa alitoroka kusikojulikana jeshi la polisi lilifanya mako mkali na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa tarehe 21 mwezi huu katika kisiwa cha Lubalagaza"