BABA AUAWA KIKATILI MBELE YA MKE NA WATOTO WAKE NA WASIOJULIKANA

0

Hofu imetanda kwa wananchi wa Kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro baada ya watu wasiofahamika kumvamia mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Henry Charles (45) na kumuua kwa kumchoma kisu shingoni na mgongoni kisha kuondoka na simu mbili na kiasi cha fedha ambazo hazijafahamika.


Mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana Novemba 13, huku mke wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Editha Saileni na watoto wao Witness Henry na Wilson Henry wakishuhudia.

Akizungumzia tukio hilo Novemba 14, Editha amesema kuwa majira ya saa 4 usiku kundi la watu watatu waliokuwa wameficha nyuso zao kwa vitambaa walivunja mlango na kuingia moja kwa moja chumbani na kuanza kumshambulia mume wake huku wakimtaka atoe pesa alizoweka kwenye suruali.

Editha amesema watu hao waliwaonya na watoto wasipige kelele hivyo alichukua suruali yenye pesa na kumpa.

"Wakati mwanangu anatoa suruali kumbe tayari wale watu walishamchoma kisu mume wangu na kumburuza hadi nje ya nyumba na kisha kukimbia.

“Nilipotoka nje na watoto nikakuta mume wangu kaanguka chini damu nyingi zikiwa zinamtoka huku akiniambia kwa kurudiarudia mke wangu nakufa," amesema Editha.

Amesema baada ya kupiga kelele majirani walitoka na wakampeleka majeruhi kwenye zahanati ya jirani hata hivyo waliwapa barua ua kwenda hospitali ya rufaa na alipofikishwa daktari alithibitisha kuwa tayari amekwishafariki dunia.

"Mume wangu mpole hana ugomvi na mtu shughuli zake ni za gereji, yaani nashindwa kujua ameuawa na kina nani na kisa nini maana hapa sebureni kulikuwa na baadhi ya vitu vya thamani kama luninga, king'amuzi lakini hawajachukua hata kimoja," amesema Editha.

Amesema kuwa baada ya mauaji hayo binti yake ambaye ameanza mitihani ya kumaliza kidato cha nne alichukuliwa na baadhi ya jamaa kwa ajili ya kumnasihi ili aweze kufanya mitihani yake.

SOMA ZAIDI>>>>>

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top