Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema matukio hayo yametokea mwezi wa tisa hadi wa kumi mwaka huu ambapo katika tukio la kwanza Happiness Amos mwenye miaka 22 anashikiliwa kwa kuiba mtoto wa miezi mitatu aliyemuiba kanisani wakati ibada ikiendelea.
Katika tukio la pili kamanda Mutafungwa amesema wanamtafuta mwanaume mmoja anayedaiwa kuiba mtoto wa miezi sita kwa kumuhadaa mama yake ambaye ni mama lishe kwa kuomba simu na kujifanya anaongea na mama wa mtoto huyo kisha kutokomea na mtoto na kwenda kumtelekeza kwenye nyumba ya mtu
Katika tukio lingine kamanda Mutafungwa amesema wanawake wawili ambao ni Pendo Embasy na mwenzake jina linahifadhiwa wanashikiliwa kwa wizi wa Watoto wawili wenye umri wa miezi sita na nane na kwamba upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani
Kufuatia matukio hayo ya wizi wa Watoto jeshi la polisi limetoa wito kwa wazazi kuwa makini na Watoto wao huku likiwaonya wanawake wenye matatizo ya uzazi na kuwataka kutumia njia sahihi za kupata Watoto na siyo kuwaiba
‘Wazazi na walezi kuweni makini na malezi ya Watoto wenu muache uzembe wa kumwamini kila mtu na kuwatelekeza Watoto bila uangalizi wa karibu na wanaotafuta watoto tumieni njia sahihi za Kwenda hospitali kupata dawa siyo kuiba Watoto’
JE! UNGETAMANI KUFANYA BIASHARA MTANDAONI? TAZAMA VIDEO HII