BWANA HARUSI ATINGA KWENYE SHEREHE YA HARUSI YAKE NA JENEZA

0

 

Video fupi ya mtandaoni iliyoshirikiwa na @tobz88 imeonyesha wakati bwana harusi akizua kisanga kufika kwenye harusi yake akiwa ndani ya jeneza.

Wakati wageni na bibi harusi mrembo walikuwa wakisubiri, wapambe wake waliwasili wakiwa wamelibeba jeneza jamaa akiwa ndani.

Katika kanda ya TikTok iliyosambaa kwa kasi, baada ya kuweka jeneza chini nyuma ya bi harusi, walilifungua, na mwanaume huyo akatoka kwa upole. 

Harusi hiyo, ambayo ilifanyika kando ya mto, ilikuwa na wageni wengine waliokuwa wakipiga picha wakitumia simu zao ili kunasa matukio hayo ya ajabu.

Watu wengi waliotoa maoni yao kuhusu video hiyo walieleza kushangazwa na harusi hiyo isiyo ya kawaida.

 Wengine walisema kwamba kamwe hawatashiriki katika hafla kama hiyo. 
Hii hapa video yenyewe
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top