Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP. Janeth Magomi imesema moto huo ulitokea majira yaa saa mbili na nusu usiku wa Novemba 23,, 2022 metokea jana Novemba 23,2022 katika bweni lililokuwa na watoto 32.
Amesema, “Polisi inafanya uchunguzi wa tukio la moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika ulioteketeza bweni la kituo cha kulelea watoto walemavu Buhangija cha Shinyanga mjini na kusababisha vifo vya watoto wakike watatu.”
Kamanda Magomi amewataja waliofariki katika tukio hilo kuwa ni Caren Mayenga (10), Niliam Limbu (12) na Catherine Paulo (10) ambao ni Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi Buhangija.
CHANZO;EDMO BLOG
USIPITWE NA VIDEO HII ,NAMNA YA KUTENGENEZA PESA MTANDAONI